2013-04-24 09:41:29

Tafakari juu ya Mzawa wa Bikira Maria- Padre Darius Kowalczyk


Padre Darius Kowalczyk , katika tafakari yake ya 26 juu ya Katekismu Mpya ya Kanisa Katoliki, wiki hii ameangalisha katika Nafsi ya pili ya Utatu Mtakatifu , ambayo tunakiri Bwana kumwilishwa, kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. . Baba Mwana wa milele alitungwa mimba ndani ya tumbo la Bikira Maria kwa uwezo wa Roho Mtakatifu na kuzaliwa.
Na hivyo , Kateksimo inatufahamisha juu ya msingi wa imani kwa Mwana aliyezaliwa na Bikira Maria, Yesu Kristo (n. 487). Kwa hiyo, Kanisa, linakiri kwamba Yesu Kristo ni binadamu Mtakatifu mwenye asili mbili: asili ya Mungu na asili ya ubinadamu. Hivyo basi Kanisa linakiri kwamba "Maria ni kweli Mama wa Mungu (Theotokos)(CCC, 495). Na hivyo tunamzungumzia Mama wa Mungu kwa sababu Mungu akawa mtu kwa wakati fulani katika historia ya binadamu kupitia kwake Bikira Maria.
Kanisa pia humwadhimisha Maria kama "Bikira milele,"likikiri kwamba ubikira wa Maria ni wa kweli na ni wa daima. Kateksimu inaeleza kwamba, kutunga mimba katika hali ya ubikira ni alama hai kwamba, ni kweli alikuwa Mwana wa Mungu" (n. 496). Basi, ubikira wa Maria hudhihirisha mpango Mungu wa kumwilisha mwana wake (n. 503). Vivyo hivyo, ubikira, unakuwa ni ishara inayo onyesha kuzaliwa kwetu upya katika maisha ya milele, si kwa mapenzi ya mwili wala kwa mapenzi ya mtu, bali mapenzi ya Mungu" (Yn 01:13) (cf. CCC, 505).

Malaika alimsalimu Mariaā€¯ umejaa neema". Katika mapito yote ya uwepo wa Kanisa, limeongozwa na Roho Mtakatifu ili ukweli wote ujulikane kwamba Bikira Maria alijawa neema kamili , ikionyesha pia Maria hakuwa na dhambi. Mama wa Mungu - katika mtazamo wa mastahili ya Mwana wake , alikingiwa kila asili ya doa la dhambi ya asili" (CCC, 491).
Kwa njia hii Mungu alimchagua Maria kuwa Mama wa Mwana wake, na si Maria aliyefanya uchaguzi huo. Na moja ya majibu yake yanayonyesha kweli huo, Mimi ni mjakazi wa Bwana, basi, na iwe kwangu kama ulivyosema (Lk 1.37-38).








All the contents on this site are copyrighted ©.