Papa atoa wito wa kuachiwa huru Maaskofu waliotekwa nyara Syria.
Papa Francis, Jumatano hii mara baada ya katekesi yake, alitoa wito wa amani kwa taifa
la Syria na kwa ajili ya kuachiwa huru, Maaskofu wawili wa Kanisa la Kiotodosi la
Syria, waliotekwa nyara mapema wiki hii.
Maaskofu hao ni eneo la Aleppo, Askofu
Mar Gregorios Ibrahim wa Kanisa la Kiotodosi la Siro na Askofu Paulo Yazigi wa Kanisa
la Kiotodosi la Kigriki ,ambao walitekwa nyara wakiwa nchini mwao Syria, wakati
wakitimiza utume wao wa kuhudumia wahitaji. Dreva wa Maaskofu hao aliuawa.
Akiwakumbuka,
Papa amewaomba waamini kuwakumbuka kafara hao katika sala, na kumwomba Mungu aangaze
nuru yake katika mioyo ya watekaji, ili iweze kulainika na kuwaachia huru mateka.
Na kurudia tena ombi lake la wakati wa adhimisho la Pasaka kwa mwaka huu,ambamo aliomba
kusitishw kwa umwagaji wa damu isiyokuwa na hatia, na utoaji wa msaada muhimu wa ubinadamu
kwa watu wanaozingirwa na hali ngumu za kipeo cha kisiasa.