Msingi wa maadili na kipimo cha jamii, ni mahitaji msingi katika maendeleo endelevu
Umuhimu wa kufuta umaskini kama ulivyo azimiwa katika Malengo ya Maendeleo Endelevu
(SDGs) si tu hitaji la kutimiza maazimio ya Mkutano wa Rio+ 20, lakini kimsingi
, kuna hitaji la kuzingatia maadili msingi katika kushughulikia namna nyingi za umaskini
wa sasa katika familia ya binadamu na chaguo linalo lenga kukuza udugu na amani
. Huu ni uchaguzi wenye upendeleo katika kufanikisha juhudi za kutokomeza umaskini
kupitia utendaji wa maendeleo endelevu, wenye kuzingatia msingi wa maadili na kipimo
cha jamii. Ni kauli ya Askofu Mkuu Francis A. Chillikutt, Nunsio na mtazamaji
wa Kudumu wa Jimbo la Papa katika Umoja wa Mataifa, wakati akihutubia mkutano wa
kidharura wa kikundi cha utendaji kwa ajili ya ufanikishaji Maendeleo endelevu ya
Millenia, siku ya Jumatatu ya 18 April 2013. Mkutano uliofanyika kwa nia za kubadilishana
mawazo juu ya ufutaji wa ufukara duniani. Askofu Mkuu Chillikutt alisema, kutokomeza
umaskini lazima kwanza , kunahitaji uelewa katika mitazamo ya usawa katika utu wa
kila mmoja na kila binadamu. Na zaidi sana, juhudi hizo zinapaswa kuongozwa na kanuni
za sheria ya asili, yenye kuvuvia maamuzi ya kisiasa , kisheria na kiuchumi na mbinu
za utendaji katika sheria za kimataifa. Ni kuyaweka maendeleo yote ya binadamu,
kama kituo kikuu cha juhudi zote za kutokomeza umaskini na uelewa sahihi juu ya umaskini
na njia bora za kufuta umaskini huo. Malengo ya maendeleo ya endelevu, kwa hiyo,
yanahitaji umuhimu wa utu na heshima ya binadamu kupewa kipaumbele, kwa mujibu wa
kutambua maamuzi na kanuni ya kwanza ya maendeleo endelevu, kama ilivyo tolewa na
Mkutano wa Rio, 1992, kwa ajili ya uhamasishaji wa mipango ya maana ambayo ni sikivu
katika mahitaji ya kila mtu na jamii. Ili kupitisha malengo ya hatua hiyo yenye
mtazamo wa ubinadamu unaozingatia hasa watu maskini na wale walio pembezoni mwa jamii,
ambao ni wengi waliokumbwa na wanapaswa kufaidika zaidi - ni lazima sauti yao isikilizwe
wakati wa kupanga mipango na utekelezaji.
Askofu Mkuu aliendelea kuzungumzia
umaskini unaotokana na watu kutengwa na wengine, katika maisha ya kiuchumi, kijamii,
kisiasa na kitamaduni, watu hao wakiwekwa nje ya jamii wanamoishi kama familia moja
ya binadamu, wakionekana kama wao hawawezi hawana uwezo wa kuendeleza yaliyo mazuri,
na hivyo hunyima fursa muhimu kushiriki wao wenyewe , familia zao na jamii zao,
katika maendeleo endelevu. Askofu Mkuu Chillikutt, katika mitazamo hiyo, amesema,
juhudi za kuwabagua maskini katika mipango ya utendaji , inakuwa na maana kuwanyima
watu maskini mahalia, sehemu yao halali katika maisha ya familia ya binadamu, na katika
matumaini na ndoto za mafanikio yao, ambayo yote mizizi yake imesimikwa katika ubinadamu
wetu wa kawaida, na ambayo hakuna hata nchi moja, watu au utamaduni , wanaoweza
kudai wana haki kipeee ya umiliki. Alikumbusha mkutano kwamba, watu wote, kwa
sababu ya uanachama wao katika familia ya binadamu, huwa na haki ya uzaliwa na haki
ya kunufaika na urithi huu wa kawaida, kuwa ni haki na wajibu wao, kushiriki katika
kurutubisha urithi huu mkubwa wa dunia.. Na kwamba mwelekeo wa kutaka kutenga baadhi
ya jamii maskini kwa sababu za kutokomeza umaskini, unaweza kuvunjwa kwa njia
ya kuwashirikishwa maskini hao , katika utendaji wote wa kiuchumi, kijamii, kisiasa
na kiutamaduni, kwa maana ya kuvunja vikwazo vyote, na wote kuingizwa, kila mmoja
akiwa na stahili ya kupata marupurupu na faida zote kwa gharama za wote. Askofu
Mkuu Chillikutt alibaini , kutengwa kwa jamii maskini , hukuzwa na ubinafsi katika
urithi wa pamoja ya binadamu, kiakili na kiasili hasa kwenye haki za biashara za
serikali, na hivyo hujenga usugu wa kiuchumi na siasa tegemezi. Na kwamba, mipango
ya kuwahirkisha wote , kwa upande mwingine, unapata maana kuwakaribisha maskini kushiriki
katika mifumo yote ya kiuchumi, kijamii, kisiasa na kiutamaduni kama washirika kamili,
na kujenga uwezo wao, ili waweze kuchukua kiti chao katika mezani ya wote, kwa usawa
kamili , hivyo kwamba masoko ya kiuchumi, yanakuwa ni kwa ajili ya faida ya wote.
Mtindo huu wa ushirikishaji unapata maana ya kweli ya ubinadamu unaozingatia,
mbinu ya kuondoa umaskini na msada unao hakikisha kwamba malengo ya maendeleo endelevu,
inakuwa mfano wa kuigwa kwa ajili ya kukuza ushirikiano wenye kuzingatia uzoefu na
hekima za wale ambao kila siku wanakabiliwa na hali halisi za changamoto za umaskini
na pia ujasiri na uvumilivu wa watu hao.