2013-04-24 08:52:50

Jifunzeni kutoka kwa Bikira Maria kutambua sauti ya Kristo na kuifuata!


Baba Mtakatifu Francisko anaendelea kupata wafuasi wengi katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii ujulikanao kama twitter. Takwimu zinaonesha kwamba, hadi sasa kuna wafuasi takribani millioni sita ambao wanamfuata katika akaunti yake. Katika lugha ya Kiingereza kuna jumla ya wafuasi millioni mbili na laki nne. Taarifa zinaonesha kwamba, wafuasi wake wanaotumia lugha ya Kihispania kwa sasa wameanza kuongezeka maradufu na kufikia wafuasi millioni mbili na laki nne na arobaini na sita elfu.

Baba Mtakatifu Francisko siku ya Jumanne, tarehe 23 Aprili 2013 katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mtandao wa twitter anasema kwamba, Bikira Maria ni mwanamke aliyethubutu kusema "Ndiyo", awasaidie waamini kutambua sauti ya Kristo na kuifuata.

Baba Mtakatifu bado anafanya rejea kwenye Maadhimisho ya Jumapili ya Nne ya Kipindi cha Pasaka, maarufu kama Jumapili ya Kristo Mchungaji mwema, Siku ya kuombea miito mitakatifu ndani ya Kanisa.







All the contents on this site are copyrighted ©.