Papa: Hakuna nafasi ya biashara dini' katika Ufalme wa Mungu
Mapema Jumatatu, Papa Francis aliwaasa,wanaotafuta manufaa binafsi kupitia mgongo
wa jamii au dini kwamba , katika dini hakuna nafasi au ngazi ya kupandia kwa nia ya
kutaka kujinufaisha mwenyewe kimaslahi au kimamlaka. Papa alieleza wakati akiongoza
Ibada ya Misa katika Kikanisa cha Mtakatifu Marta ndani ya Vatican , ibada iliyohudhuria
na Wafanyakazi na waandishi wa habari kutoka Ofisi ya Habari ya Vatican , Redio Vatican
na Kituo cha kurushia cha St Maria di Galeria, wakiongozwa na Homilia ya Papa,
ilitazamisha katika Injili, ambamo Yesu anawaambia wanafunzi wake kuwa, yeyote
asiyeingia kupitia Mlango wa zizi , si mchungaji, lakini ni mwizi na mnyang'anyi.
Hii ina maana yeyote anayetafuta kupata faida zake binafsi,kwa mgongo wa dini na
jamii, kupitia njia za uongo na udanyanyifu, hana nafasi katika ufalme wa Mungu.
Lango pekee la kuingia Ufalme wa Mungu, na Kanisa, ni kuliishi Neno la Injili ya
Yesu mwenyewe.
Papa aliwataja walaghai na mafisadi , ambao wamo hata katika
jamii ya Kikristo, wale wenye ubinafsi wa kujiangalia wenyewe tu, kupitia kupitia
milango mingine mbalimbali kuwa ni wezi na majambazi.