2013-04-22 10:57:56

Vijana kuweni na uadilifu na Shangilieni jina la Yesu- Papa Francisko


Hotuba ya Papa wakati wa Sala ya Malkia wa Mbingu , imesema, "Vijana mnahitaji kukomalia uadilifu wa hali ya juu, na kulishangilia jina la Yesu".

Kujiamini , mshikamano wa dhati na kina cha uelewa, ni msisitizo uliotolewa na Papa Francisko, wakati wa sala ya Malkia wa Mbungu, Jumapili iliyopita , ambamo Kanisa pia liliadhimisha Siku ya Dunia ya Kuombea Miito. Papa alizungumzia mahusiano ya urafiki unaowezesha kuwa na Yesu kwa kuisikiliza sauti yake. Alitumia mfano wa mchungaji na kondoo wake, kama ilivyoadikwa katika Injili ya Yohane , Injili iliyosomwa Jumapili. Na pia baadaye alielekeza mawazo yake katika hali ya maisha ya watu wa Venezuela, na wale walioathirika na tetemeko, nchini China na kwa Padre Niccolo 'Rusca, aliyetangazwa kuwa Mwenye Heri, siku ya Jumapili. Aliwakumbusha waliokuwa wakimsikiliza kwamba, "Yesu anataka kuanzisha uhusiano na wote wanao mridhia, kujenga uhusiano thabiti kama ilivyo kwa Yeye mwenyewe na Baba yake , walivyo katika ushirika wa karibu sana."
Papa Francesco, alieleza na kunukuu maneno Yesu katika Injili ya Yohane , "kondoo zangu husikia sauti yangu, na nami nawajua na hunifuata mimi... hakuna mtu atakayeweza kuwatoa katika mkono wangu, wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu. katika aya hizi nne kuna ujumbe kamili wa Yesu:"Yeye anatuita kushiriki katika uhusiano wake na Baba, na hili ni uzima wa milele."
Papa aliendelea kuutaja mfano wa Kondoo na Mchungaji kuwa ni mfano mzuri wa ajabu, ni sauti ya siri ya kuvutia inayotuita tangu tukiwa bado tumboni mwa mama zetu, kujifunza kuitambua sauti yake na ile ya Baba. Ni sauti ya kujua upendo au ghadhabu, upendo au ubaridi. Sauti ya Yesu ni ya kipekee! Yenye kutuongoza sisi kujifunza kutofautisha, yenye kutongoza katika njia ya maisha,njia ambayo inakwenda zaidi ya dimbwi la kifo. "
Papa Francisko anasema "hii ni siri kubwa, na si rahisi kuelewa"....."... ni hisia za kuvutiwa na Yesu, sauti yake ikileta jotojoto la uhai mioyoni mwetu, na hivyo tunapaswa kumshukuru Mungu Baba, ambaye ameweka ndani yetu hamu hii ya upendo, ukweli, uzuri maisha ... na hivyo kwetu Yesu anakuwa ni kila jambo katika ukamilifu wake... " Papa alikamilisha hotuba hii na ombi kwa Bikira Maria atusaidie kuitambua vyema sauti ya Yesu na kumfuta Yeye katika njia ya maisha ya milele.
Wito kwa Taifa la Venezuela
Baada ya sala ya Malkia Mbingu, Papa alielekeza mawazo katika Venezuela, na kutolea sala kwa matumaini kwamba , Mungu atawawezesha kupata njia ya amani, haki na maelewano , ili kuondokana matatizo makubwa yanayolikumba taifa hilo kisiasa. Alitoa wito kwa watu wapendwa wa Venezuela, hasa kwa viongozi na wasiasa, idara za serikali na vyama vay Kisiasa, kukataa kwa uthabiti, aina yoyote ya vurugu, na kuanzisha mazungumzo katika misingi ya ukweli huku wakitambua kuheshimiana, na kwa pamoja kushirikiana katika kufanikisha mema na upendo kwa taifa zima la Venezuela. Aliwaomba wafanye kazi kwa maridhiano, amani na kuwaweka katika mikono ya Mama yetu wa Coromoto. "
Tetemeko la ardhi
Pia Papa alipeleka mawazo kwa walio athirika na tetemeko la aridhi, Kusini-Magharibi mwa China.
Na kisha Papa alimkumbuka tukio la kutajwa kuwa Mwenye Heri, Padre Nicolò Rusca wa Sondrio, Valtellina, kuhani aliyeishi karne ya kumi na sita na kumi na saba, aliyeuwa katika mapambano ya kisiasa na kidini ya wakati huo barani Ulaya. Alitolea shukurani kwa Bwana kwa ajili ya ushahidi wake. "
Salaam za ujumla
Papa pia alitoa salamu joto joto kwa mahujaji wote ambao walifika kumsikiliza toka nchi mbalimbali: familia, makundi ya kikanisa na vyama mbalimbali vya kikanisa na jumuia, hasa kikundi cha vijana kutoka Jimbo la Venice. Aliwakumbusha wavulana na wasichana kwamba, utendaji wao wa kimaisha kwa uthabiti uzingatie maadili.
Siku ya Dunia ya Kuombea miito
Na Siku ya Dunia ya Kuombea Miito, ni adhimisho lililoanzishwa miaka hamsini iliyopita kwa uvuvio wa Papa Paulo VI, Papa alitoa mwaliko maalum kwa kila mtu, kutolea sala zake kwa namna ya kipekee , ili Bwana, atume wafanyakazi wengi shambani mwake.
Papa alikamilisha na sala kwa Mtakatifu Hannibal Maria wa Francia, Mtume wa sala kwa ajili ya miito, akisema, leo hii anatukumbusha tena ahadi hii muhimu. Mwisho Papa aliwatakia wote, Jumapili njema.








All the contents on this site are copyrighted ©.