2013-04-22 15:14:50

Redio Maria (FM) kuzinduliwa Kinshasa.


Baada ya majaribio ya kitalaam mwezi Novemba 2012, Muadhama Kardinali Laurent Mosengwo Pasinya , wa Jimbo Kuu la Kinshasa, anatazamia kuzindua rasmi, Kituo cha Redio Maria Kinshasa, kitakachokuwa kikitoa matangazo yake katika masafa ya FM 89.9 na kusikika katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Redio hii ni sauti ya Kanisa Katoliki, ambayo miezi miwili iliyopita, iliingizwa kimajaribio kwenye mfumo wa Redio Maria, ambao tayari husikika katika mataifa kadhaa ya Afrika.. Togo, Rwanda na Burundi na Tanzania na Congo Brazaville.
Kituo hicho kipya , pia kitakuwa kinachota matangazo kutoka Redio Vatican , kama Rendezvous Afrika, kila siku, hasa ikitoa habari za Kanisa,na pia habari zilizoandikwa katika magazeti . Aidha itakuwa ikitoa kwa kina mafundisho ya Jamii ya Kanisa Katoliki.
Pia kuna maelezo kwamba, habari za maisha ya kila siku ya jamii parokiani, zitaendelea kutolewa na Kituo kingine cha utangazaji cha Redio Maria “Mama wa Elikaya”, kinacho julikana kama kituo cha Matumaini, kilichozinduliwa mwaka 1995. Kituo hicho hutoa matangazo yake katika lugha ya Kifaransa na kilingala , lugha zinazotumika zaidi katika Liturujia za Kanisa Katoliki katika Jimbo Kuu la Kinshasa.
Inatajwa mkoa Kinshasa una zaidi ya vituo vya redio 60 ambavyo matangazao yake husikika hata nje ya mipaka ya DRC.







All the contents on this site are copyrighted ©.