Imani vuguvugu hujenga makanisa madogo lakini si Kanisa la Yesu - Papa Francesco.
Wakristo wenye imani haba au wenye imani vuguvugu, hujenga kanisa katika kipimo
chao wenyewe na hivyo hilo si kanisa la Yesu, Papa Francesco, alieleza mapema siku
ya Jumamosi, wakati wa Ibada ya Misa, aliyoadhimisha akiwa na watu wa kujitolea
kutoka Zahanati za Watoto ya Mtakatifu Marta . Ibada ilifanyika katika Kikanisa cha
Domus Sanctae Martha ndani ya Vatican. Baadhi ya washiriki wakiwa Mabinti wa Upendo
wa Paolo wa Mtakatifu Vincent de, Jumuiya ambayo kwa muda wa miaka kwa miaka 90, imekuwa
ikisaidia watoto na familia zao bila ubaguzi wa kidini wala utaifa. Papa aliongoza
Ibada hiyo akisaidiwa na watoto wawili wa kiume. Katika homilia yake alitazama
zaidi Jumuiya za kwanza za Kikristo, kwamba baada ya mateso, walikiishi kipindi cha
amani , wakiimarishana , kutembea pamoja na kukua katika kumcha Bwana, wakiimarishwa
na faraja ya Roho Mtakatifu". Papa alieleza kwa kulitazama somo kutoka Matendo ya
Mitume akisema, “hiii ni hewa halisi ambamo Kanisa linatakiwa kuishi na kupumua. Ni
wote wa kutembea mbele ya Mungu na uwajibikaji. Papa alihoji iwapo maisha ya
Kanisa la Yesu, yana maana ya uwepo tu wa hisia ndogo ndogo za kuabudu, hisia zilizojaa
mashakamashaka kwa uwepo wa Mungu. Alitoa jibu Hapana . Kanisa halipaswi kutembea
katika hali hiyo ya kushakia uwepo wa Mungu, na wala kuwa na utendaji mbovu wala kuwa
maamuzi yasiyomfaa binadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Wakristu Kama
Kanisa mbele ya Mungu, muda wote, ni wakati wa furaha inayobubujika kutoka kwa Roho
Mtakatifu, Zawadi kubwa iliyotolewa na Bwana , inayowezesha Kanisa kusonga mbele katika
imani thabiti ya Injili . Hivyo Waristu hao wenye imani vunguvugu, nguvu yao haiwezi
kutegemewa kujenga kanisa thabiti la Bwana, kwa kuwa upepo kidogo ukivuma huondoka
njiana kupotelea gizani. Papa Francesco, alipeleka mawazo yake kwa Wakristu wengi
, ambao kwa wakati huu wanaendelea kulishuhudia jina la Yesu hata katika hatari za
vifo, akisema hawa si Wakristu hewa, lakini wapo na tunaishi nao wakitembea na Yesu
katika njia ya Yesu. Wako tayari kutoa jibu kama la Petro alipoulizwa na Bwana:
'Wewe pia unataka kwenda? Simoni Petro alijibu: `Bwana, Twende kwa nani ? Wewe unayo
maneno ya uzima wa milele . Hivyo katika kundi kubwa, bado kuna wale ambao wanajua
vizuri kabisa kwamba hawawezi kwenda mahali pengine, kwa sababu tu Yeye, Bwana, ana
maneno ya uzima wa milele. "
Papa alihitimisha homilia yake na sala: "Tuombe
kwa ajili ya Kanisa, ili liendelee kukua, kuimarika, na kutembea katika imani na
faraja ya Roho Mtakatifu. Naomba Bwana utuokoe na majaribu ya 'akili ya kawaida'
katika majaribu ya kumnung'unikia Yesu, kwa kuwa ni udhaifu na majaribu ya kashfa.."