2013-04-20 10:36:57

Ujumbe wa Papa kwa Watu waliofikwa na maafa mjini Texas, USA


Baba Mtakatifu Francisko anasema, amepokea kwa masikitiko makubwa habari za maafa yaliyotokea Magharibi mwa Texas, Marekani, wakati kiwanda cha kutengeneza mbolea kilipolipuka na kuwaka moto na hivyo kusababisha maafa makubwa hapo tarehe 18 Aprili 2013.

Baba Mtakatifu katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Tarcisio Bertone, Katibu mkuu wa Vatican kwenda kwa Askofu Joe Vasquez wa Jimbo la Austin, anamwomba kuwafikishia salam zake za rambi rambi wote waliofikwa na msiba huu mzito. Anawaombea faraja na amani wote wanaoendelea kusaidia katika maafa haya.

Taarifa zinaonesha kwamba, watu kumi na wanne wamepoteza maisha yao na wengine wengi kupata majeraha wakati wa ajali hiyo ya moto huko Texas, Marekani.







All the contents on this site are copyrighted ©.