Askofu mkuu Samuel Klèda achaguliwa kuwa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Cameroon
Baraza la Maaskofu Katoliki Cameroon katika mkutano wake wa Mwaka uliofanyika hivi
karibuni limemchagua Askofu mkuu Samuel Klèda wa Jimbo kuu la Douala kuwa Rais mpya
wa Baraza la Maaskofu Katoliki Cameroon. Askofu mkuu Klèda alipadrishwa tarehe 9 Machi
1986. Akateuliwa kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Batouri wakati wa Maadhimisho ya Jubilee
kuu ya Miaka 2000 ya Ukristo.
Amewafundisha, kuwaongoza na kuwatakatifuza Waamini
wa Jimbo Katoliki Batouri hadi mwaka 2009 alipoteuliwa na Baba Mtakatifu Benedikto
wa kumi na sita, kuwa Askofu mkuu wa jimbo kuu la Douala. Kuanzia mwaka 1997 hadi
mwaka 2010 alikuwa ni Makamu wa Rais, Baraza la Maaskofu Katoliki Cameroon. Kwa sasa
ataongoza kwa kipindi cha miaka mitatu.