2013-04-18 12:36:09

Papa anasali kwa ajili ya watu waliofikwa na maafa ya mlipuko Texas, USA


Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii maarufu kama twitter, siku ya Alhamis tarehe 18 Aprili 2013 anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kusali kwa ajili ya kuwaombea watu walioathirika kutokana na mlipuko uliotokea kwenye kiwanda cha kutengeza mbolea mjini Texas, Marekani.

Taarifa za Jeshi la Polisi zinaonesha kwamba, watu 5 hadi 15 wanahofiwa kwamba, wamefariki dunia kutokana na mlipuko huo na wengine zaidi ya watu 200 wamepata majeraha pamoja na uharibifu mkubwa wa miundo mbinu. Serikali ya Marekani inaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha mlipuko huo.







All the contents on this site are copyrighted ©.