2013-04-17 14:38:57

Yesu Kristo yuko pamoja na wafuasi wake!


Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii maarufu kama twitter anawakumbusha kwamba, kupaa kwa Yesu kwenda mbinguni hakumaanishi kutoweka kabisa, bali anaendelea kuwepo miongoni mwa wafuasi wake kwa namna mpya na kwamba, yuko karibu na kila mmoja wao.

Anasema ili kuingia katika utukufu wa Mungu kunahitaji uaminifu wa kila siku katika kutekeleza mapenzi ya Mungu, hata pale inapobidi kutolea sadaka kubwa!







All the contents on this site are copyrighted ©.