2013-04-17 14:37:12

Mshikamano wa Papa Francisko na wananchi wa Iran na Pakistan waliokumbwa na tetemeko la ardhi


Baba Mtakatifu Francisko kwa mara nyingine tena ameonesha moyo wa upendo na mshikamano wa dhati kwa wananchi wa Iran na Pakistan waliokumbwa na tetemeko la ardhi na hivyo kusababisha maafa makubwa pamoja na uharibifu wa miundo mbinu. Anamwomba Mwenyezi Mungu aweze kuwafariji wale waliofikwa na msiba wa kuwapoteza ndugu, jamaa na marafiki ili waweze kufarijika kwa sala zake.

Anawaombea majeruhi waweze kupona haraka na kuendelea na shughuli zao za kila siku. Kwa namna ya pekee, Baba Mtakatifu anasema kwamba, yuko pamoja na wote wanaoteseka kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea siku ya Jumanne tarehe 16 Aprili 2013.







All the contents on this site are copyrighted ©.