2013-04-16 12:06:31

Askofu mteule Michael W. Banach ateuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Papua New Guinea


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Monsinyo Michael W. Banach kuwa Balozi mpya wa Vatican nchini Papua New Guinea. Itakumbukwa kwamba, aliteuliwa na Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, kuwa Askofu mkuu tarehe 22 Februari 2013. Alizaliwa kunako tarehe 19 Novemba 1962. Baada ya masomo na majiundo yake, akapadrishwa tarehe 2 Julai 1988.







All the contents on this site are copyrighted ©.