2013-04-15 09:45:00

Utangazaji wa Injili na Ushuhuda makini ni sawa na chanda na pete!


Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii maarufu kama Twitter anawakumbusha kwamba, haiwezekani kamwe kutangaza Injili ya Yesu bila ya kuwa na ushuhuda unaomwilishwa katika uhalisia wa maisha ya kila siku.

Anasema, kuabudu maana yake ni kujifunza kukaa pamoja na Mungu, kujivua miungu uchwara iliyojificha ndani mwao na kutoa kipaumbele cha kwanza cha uwepo wa Mungu katika maisha.







All the contents on this site are copyrighted ©.