Papa aunda tume ya Makardinali kuangalia uongozi wa Kanisa la Kiulimwengu
Baba Mtakatifu Francisko kwa kuzingatia ushauri uliotolewa na Makardinali katika mikutano
yao elekezi iliyofanyika kabla ya uchaguzi wa Papa Mpya ameamua kuunda Tume ya Makardinali
watakaomshauri kuhusu shughuli za uongozi wa Kanisa la Kiulimwengu pamoja na kupembua
kwa kina na mapana Waraka wa Kichungaji Pastor Bonus, Mchungaji mwema unaohusiana
na masuala ya Ofisi za Vatican.
Kwa mara ya kwanza tume hii itakutana kuanzia
tarehe 1- 3 Oktoba 2013. Tangu wakati huu, Baba Mtakatifu Francisko ataanza kuwasiliana
moja kwa moja na wahusika kwa ajili ya kupata ushauri makini.