2013-04-13 09:34:42

Endeleeni kumwombea Papa Francisko katika maisha na utume wake!


Kardinali Polycarp Pengo, Rais wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika na Madagascar, SECAM anaendelea kumwombea Baba Mtakatifu Francisko ili Mwenyezi Mungu aweze kumlinda na kumwimarisha katika imani, matumaini na mapendo anapotekeleza utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro. RealAudioMP3

Anamwombea afanikishe malengo na nia njema zilizoko moyoni mwake, lakini zaidi aweze kuwaimarisha ndugu zake katika imani kwa Kristo na Kanisa lake, hasa zaidi maskini, wanaosukumizwa pembezoni mwa Jamii na wote waliokata tamaa kutokana na madhulumu mbali mbali.

Kardinali Polycarp Pengo anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kuendelea kumwombea Baba Mtakatifu Francisko katika maisha na utume wake.







All the contents on this site are copyrighted ©.