2013-04-12 09:21:05

Tuzo katika kuhamasisha uelewa makini wa Mfundisho Jamii ya Kanisa ili kuyatakatifuza malimwengu


Kardinali Domenico Calcagno, Rais msimamizi wa urithi na mali ya Vatican, Alhamisi, tarehe 11 Aprili 2013 ametoa tuzo ya kwanza kutoka kwenye Mfuko wa Kipapa wa Centesimus Annus kwa washindi wa kimataifa katika masuala ya kiiuchumi na kijamii. Zawadi ya kwanza imetolewa kwa waandishi wa vitabu vinavyojadili kuhusu: uraia, uhamiaji na dini.

Kingine kinajadili masuala ya majadiliano ya kimaadili mintarafu imani ya Kikristo. Hivi ni vitabu ambavyo vimeandikwa na Professa Julio Luis Martines. Kitabu kingine ni kile kilichoandikwa na Professa Stefano Zamagni kinachozungumzia uchumi na mafao ya wengi.

Tuzo la Uchumi na Jamii lilianzishwa na Mfuko wa Kipapa wa Centesimus Annus ili kuhamasisha uelewa makini wa Mafundisho Jamii ya Kanisa katika mchakato wa kuyatakatifuza malimwengu, changamoto kubwa inayotolewa na Mama Kanisa kwa waamini walei wanaotoa huduma na taaluma katika medani mbali mbali za maisha.







All the contents on this site are copyrighted ©.