Sudan ya Kusini yatembelewa kwa mara ya kwanza na Rais Omar Al Bashir
Rais Omar Al Bashir wa Sudan Kongwe, Ijumaa, tarehe 12 Aprili 2013, kwa mara ya kwanza
tangu Sudan ya Kusini ilipoamua kujitenga na kuwa nchi Huru kunako mwaka 2011 amewasili
mjini Juba, Sudan ya Kusini.
Lengo la ziara hii ya kikazi wanasema wachunguzi
wa masuala ya kisiasa ni kutaka kurudisha hali ya kawaida kati ya nchi hizi mbili
ambazo kwa siku za hivi karibuni zilijikuta zikiingia katika kinzani kuhusu uzalishaji
wa nishati ya mafuta.
Suluhu ya mgogoro huu ilifikiwa hapo tarehe 12 Machi
2013 kwa makubaliano kwamba, uzalishaji na usafirishaji wa nishati ya mafuta kutoka
Sudan ya Kusini uendelee kama kawaida.