2013-04-11 10:20:27

Yatoeni maisha yenu kwa Yesu ili awaletee utulivu na furaha ya kweli!


Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwa watumiaji wa mitandao ya Kijamii maarufu kama twitter aliyouandika Jumatano, tarehe 10 Aprili 2013, anawakumbusha waamini kwamba, kuwa Mkristo hakumaanishi kufuata tu sheria, bali ni kumwachia Yesu Kristo kuwa ni mmiliki wa maisha yao, ili aweze kuwaletea mabadiliko.

Anawataka waamini kutenda kama watoto wateule wa Mungu, kwa kutambua kwamba, anawapenda na kwa njia hii maisha yao kwa hakika yatakuwa mapya yakisheheni utulivu wa ndani na furaha ya kweli.







All the contents on this site are copyrighted ©.