2013-04-11 11:03:17

Moneyval inaendelea kujadiliana na Vatican ili kudhibiti vitendo vya utakatishaji wa fedha


Vatican bado inaendelea kujadiliana na Moneyval, Tume ya Wataalam wa fedha na udhibiti wa utakatishaji wa fedha pamoja na kugharimia vitendo vya kigaidi ya Umoja wa Ulaya. Tume hii imeamua kwamba, taarifa endelevu ya masuala ya fedha za Vatican itawasilishwa mwishoni mwa Mwezi Desemba 2013.

Vatican pia imeomba kuwasilisha taarifa pana zaidi si tu kwa vigezo vilivyokuwa vimebainishwa na Tume hii. Lengo ni kuonesha hatua ambazo zimechukuliwa na Vatican hadi sasa katika kudumisha ukweli na uwazi kwenye masuala ya fedha ili kudhibiti utakatishaji wa fedha pamoja na kugharimia vitendo vya kigaidi, mambo yanayoweza kupenyeza hata kwenye taasisi kama hii.

Itakumbukwa kwamba, taarifa ya fedha za Vatican ilikaguliwa na kuthibitishwa na Tume hii hapo Julai 2012. Vatican inapenda kuendeleza majadiliano haya ili kuimarisha mchakato wa kudhibiti vitendo vya utakatishaji wa fedha pamoja na kugharimia matukio ya kigaidi.







All the contents on this site are copyrighted ©.