Kuna watoto zaidi ya 2000 waliopotezana na wazazi wao katika mapigano Jamhuri ya Watu
wa Afrika ya Kati
Chama cha Msalaba Mwekundu Kimataifa kinakadiria kwamba, kuna jumla ya wakimbizi 22,
100 kutoka Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati na asilimi arobaini ya wakimbizi hawa
ni watoto wenye umri kati ya miaka miwili hadi kumi na minne, waliopotezana na wazazi
wao baada ya machafuko ya kisiasa nchini humo hivi karibuni.
Takwimu za Chama
cha Msalaba Mwekundu Kimataifa zinaonesha kwamba, kuna walau watoto ambao ni wakimbizi
wapatao laki mbili waliokuwepo kati ya mwezi Januari na Februari mwaka huu. Idadi
hii imeongezeka maradufu kutokana na mapambano ya vita kuzidi kupamba moto nchini
Afrika ya kati. Hadi sasa wachunguzi wa mambo wanasema, hali bado ni tete!