2013-04-08 12:09:08

Askofu mkuu Brian Udaigwe ateuliwa na Papa Francisko kuwa Balozi Mpya wa Vatican nchini Benin


Baba Mtakatifu Francisko amemteua Askofu mkuu Brian Udaigwe kuwa Balozi wa Vatican nchini Benin. Itakumbukwa kwamba, Askofu mkuu mteule Udaigwe aliteuliwa na Baba Mtakatifu mstaafu Benedikto wa kumi na sita hapo tarehe 22 Februari 2013 kuwa Askofu mkuu na Balozi wa Vatican.

Askofu mkuu mteule, alizaliwa Tiko, nchini Cameroon kunako mwaka 1964. Baada ya masomo na majiundo yake ya kipadre, alipewa daraja takatifu kunako mwaka 1992. Alianza kushiriki utume wa Kidiplomasia mjini Vatican kunako mwaka 1994. Tangu wakati huo ametekeleza utume wake nchini Zimbabwe, Pwani ya Pembe, Haiti, Bulgaria, Thailand na Uingereza.







All the contents on this site are copyrighted ©.