2013-04-05 11:57:29

Changamoto zinazoikabili Msumbiji katika mchakato wa kupambana na baa la umaskini!


Mtaalam wa kupambana na baa la umaskini kutoka Umoja wa Mataifa Bi Madgalena SepĆ¹lveda kuanzia tarehe 8 hadi 16 Aprili 2013 atakuwa na ziara ya kikazi nchini Msumbiji ili kujionea mwenyewe hali halisi kuhusu haki msingi za binadamu kwa watu wanaokabiliwa na umakini wa hali na kipato.

Atafanya upembuzi yakinifu kuhusu mikakati na sera zinazochukuliwa na Serikali katika kulinda na kutetea haki zao msingi; mapambano dhidi ya umaskini pamoja na kuangalia vikwazo wanavyokabiliana navyo katika mapambano haya. Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, Msumbiji imepiga hatua kubwa katika maendeleo ya kiuchumi, lakini bado watu wengi wanaogelea katika dimbwi la umaskini wa hali na kipato.

Umoja wa Mataifa unataka kuona ni jinsi gani Serikali inavyojitahidi kuboresha hali ya maisha ya wananchi wake, huduma za kijamii na utekelezaji wa haki msingi za binadamu kupitia vyombo vya sheria.







All the contents on this site are copyrighted ©.