2013-04-04 10:13:47

Waamini wa Kanisa la Mtakatifu Saturinus kumpokea Kardinali Onaiyekan, hapo tarehe 7 Aprili 2013 mjini Roma


Kardinali John Olorufemi Onaiyekan, Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Abuja, Nigeria, aliyeteuliwa na Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, kunako tarehe 24 Novemba 2012 ataadhimisha kwa mara ya kwanza Ibada ya Misa Takatifu katika Kanisa alilopangiwa kama Kardinali Padre, kielelezo cha huduma, umoja na mshikamano na Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Idara ya Liturujia za Kipapa inaonesha kwamba, Kardinali atakabidhiwa Kanisa la Mtakatifu Saturinus lililoko mjini Roma, Jumapili ya Huruma ya Mungu ambayo kwa Mwaka huu inaadhimishwa hapo tarehe 7 Aprili 2013.









All the contents on this site are copyrighted ©.