Jaji wa Mahakama kuu ya Kenya Willy Mutunga katika akaunti yake ya mtandao wa twitter
anasema kwamba, Mahakama kuu ya Kenya inatarajiwa kutoa hukumu ya kesi ya rufaa inayopinga
matokeo ya uchaguzi mkuu nchini Kenya, uliofanyika hivi karibuni, na kumpatia ushindi
Rais Uhuru Kenyatta, Jumamosi, tarehe 30 Machi 2013.
Wachunguzi wa masuala
ya kisiasa wanafuatilia mchakato huu wa umakini mkubwa, wakiwa bado wanakumbu kumbu
za machafuko ya kisiasa yaliyojitokeza nchini Kenya kunako mwaka 2007.