2013-03-30 08:20:51

Jumuiya ya Wayahudi wa Roma yatuma salam za Pasaka kwa Baba Mtakatifu Francisko


Baba Mtakatifu Francisko katika maadhimisho ya Pasaka ya Wayahudi, alimwandikia ujumbe wa matashi mema Rabbi Riccardo Di Segni, Mkuu wa Jumuiya ya Wayahudi mjini Roma, ambaye pia amemtumia Baba Mtakatifu Francisko ujumbe wa matashi mema kwa Maadhimisho ya Siku kuu ya Pasaka kwa Mwaka 2013.

Rabbi Riccardo Di Segni anachukua fursa hii kumshukuru Baba Mtakatifu Frncaisko kwa ujumbe na matashi mema aliyoiandikia Jumuiya ya Wayahudi inayoishi mjini Roma na kumtakia kheri na fanaka wakati wa Maadhimisho ya Siku kuu ya Pasaka ambayo kwa Mwaka huu siku zimekaribiana sana, hali inayoonesha uhusiano na tofauti zilizopo kati ya dini hizi mbili, ambazo katika historia, wakati mwingine ukajionesha katika hali ya kinzani na Jumuiya ya Wayahudi kutovumiliwa.

Kurasa hizi chungu zinaonekana kupitwa na wakati na sasa waamini wa dini hizi mbili wanafurahia matunda ya imani yao, mwaliko wa kumtolea Mwenyezi Mungu shukrani za dhati. Rabbi Di Segni anasema, anasukumwa na moyo wa heshima, urafiki na udugu ili kumtakia mema, kwa ajili ya mema yenyewe kwa kutambua tofauti zilizopo pamoja na kuendelea kuthamini moyo wa udugu.







All the contents on this site are copyrighted ©.