2013-03-30 09:38:27

Idadi ya waliofariki dunia Dar inazidi kuongezeka!


Idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na kuporomoka kwa Jengo lenye ghorofa 16, hadi kufikia Jumamosi asubuhi ni watu 17, kadiri ya taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Said Meck Sadick kwa Shirika la Habari la Reuters. Juhudi za kuokoa maisha ya watu waliofukiwa na kifusi zinaendelea, ingawa matumaini ya kuwapata wangali hai yanazidi kufifia kadiri muda unavyozidi kuyoyoma.

Kufuatia tukio hili la kusikitisha, Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania ametembelea eneo la tukio na kuhuzunishwa na maafa yaliyotokea. Ametoa agizo ya kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wahusika wakuu yaani: mjenzi, mhandisi mshauri na mhandisi wa Jiji aliyetoa kibali pamoja na mmiliki wa jengo hilo.







All the contents on this site are copyrighted ©.