2013-03-27 15:13:06

"Sitisheni vita, tafuteni suluhu ya kisiasa, ili amani na utulivu viweze kutawala tena Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati!


Baba Mtakatifu Francisko wakati wa Katekesi yake, Jumatano kwenye Uwanja wa kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican amesema kwamba, anafuatilia kwa umakini mkubwa matukio mbali mbali yanayoendelea kujitokeza huko Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati.

Anatumia fursa hii, kuwahakikishia wote wanaoteseka, ndugu na jamaa za wale waliopoteza maisha; waliojeruhiwa, waliopoteza makazi yao au kulazimika kuyakimbia; uwepo wake wa karibu kwa njia ya sala.

Anawaalika wahusika wote kusitisha mara moja vita na uporaji wa mali ya watu, ili kuanza mchakato utakaosaidia kupata suluhu ya kisiasa ili amani na utulivu viweze kurudi na kutawala tena Jamhuri ya Watu wa Afrika ya Kati, nchi ambayo kwa siku za hivi karibuni imejikuta ikiogelea katika dimbwi la kinzani na migawanyiko.







All the contents on this site are copyrighted ©.