2013-03-27 12:08:47

Papa Francisko anatwitter na watumiaji wa mitandao ya kijamii!


Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe wake kwenye mtandao wa twitter anawakumbusha waamini kwamba, ili kuendelea kuwa na Yesu, kuna haja ya kujitoa katika ubinafsi na hali ya kuiishi imani kwa hali ya kuchoka na mazoea.

Ili kuishi vyema Maadhimisho ya Juma kuu, kuna haja ya kuingia katika mantiki ya Mungu, inayofumbata upendo na majitoleo binafsi.







All the contents on this site are copyrighted ©.