Salam na matashi mema kutoka kwa Papa Francisko kwenda kwa Wayahudi wa Roma wanapoadhimisha
Siku kuu ya Pasaka
Baba Mtakatifu Francisko katika Maadhimisho ya Siku kuu ya Pasaka ya Wayahudi, amemwandikia
ujumbe wa matashi mema Rabbi Riccardo Segni, Mkuu wa Jumuiya ya Wayahudi mjini Roma,
akisema kwamba, siku chache zilizopita, walibahatika kukutana mjini Vatican, anamshukuru
kwa uwepo wake wakati alipokuwa anaanza utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro
na Askofu wa Roma.
Baba Mtakatifu Francisko anachukua fursa hii kutuma salam
na matashi mema kwa Jumuiya ya Wayahudi walioko mjini Roma wakati huu wanapoadhimisha
Pasaka ya Wayahudi, inayojulikana kama Pesach! Mwenyezi Mungu aliyewakomboa watu wake
kutoka utumwani Misri na kuwaongoza katika Nchi ya ahadi, aendelee kuwakomboa kutoka
katika kila aina ya ubaya na kuwaongoza kwa njia ya baraka zake.
Baba Mtakatifu
Francisko anawaomba Wayahudi wa Roma kumwombea na kwamba, anawahakikishia sala zake.
Ni matumaini ya Baba Mtakatifu Francisko kwamba, wataendelea kujenga na kuimarisha
uhusiano huu katika heshima na urafiki.