2013-03-26 11:24:10

Bustan Mpya yafunguliwa mjini Vatican, kivutio kikuu kwa watalii!


Bustani ambayo Mwenyeheri Yohane Paulo wa pili alimwomba Mhandisi Jacopo Meleghino kuianzisha mjini Vatican, imefunguliwa rasmi kwa watalii kuanzia tarehe 25 Machi 2013. Ni bustani yenye mvuto wa pekee, inayotoa mandhari kwa watalii kupata nafasi ya kuketi ili kushangaa kazi ya uumbaji, baada ya kuwa wamehitimisha safari ya kutembelea Makumbusho ya Vatican yenye utajiri mkubwa na urithi wa dunia.

Ukiwa kwenye bustani, unaweza kuona kwa ufasaha Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, mjini Vatican. Muda wa kutembelea Bustani hii ni kama ule wa kutembelea Makumbusho ya Vatican. Kwa wale wanaobahatika kufika Roma basi, wasikose nafasi ya kutembelea Bustani hii yenye mvuto mkubwa kwa sasa.







All the contents on this site are copyrighted ©.