2013-03-23 16:54:51

Papa Francis amtembelea Mstaafu Papa Benedikto XV1


Jumamosi, ikiwa zimepita siku kumi baada ya kuchaguliwa kwake, Papa Francis, alimtembelea Mstaafu Mtakatifu Benedikto XV1, katika makazi ya Kipapa ya Castel Gadolfo, na kupata chakula cha mchana pamoja. ziara hii ilifanyika katika hali ya faragha, kama kukidhi hamu aliyokuwa nayo, Papa mpya Francis, kumtembelea mtagulizi wake Benedikto XV1.
Tukio hili limekuwa na sura ya kihistoria ya kipekee , kutokana na kwamba kimepita kipindi cha karne nyingi bila ya kutokea tukio kama la Papa, kusalimiana na mtagulzi wake akiwa hai. Lilikuwa ni tukio jepesi binafsi, lisilokuwa na maandamano au mikusanyiko ya watu kama ambavyo imekuwa ikionekana katika siku hizi za kumpongeza Papa mpya Francis .
Papa Francis, ameonyesha kuwa na upendo wa kipekee kwa Papa Mstaafu kama kama ilivyo jionyesha mara baada ya kuchaguliwa kwake, hapo tarehe 13 March 2013, alisema, "Awali ya yote, ninapenda kutolea sala kwa ajili ya askofu wetu mstaafu, Benedict XVI. Tuombe kwa ajili yake, ili Bwana na Bikira Maria amwangalie kwa macho yao ya upendo na huruma . Hiyo inaonyesha jinsi Papa Francis anavyo mheshimu Mstaafu Papa Benedict XVI. Na mara baada ya kusalimia watu, alipiga simu Castel Gandolfo. kitendo hiki kinatajwa kuwa ni tendo la unyenyekevu na upendo, ulioshangaza Papa Mstaafu na wasaidizi wake. Nae Papa Mstaafu alisema, Bwana anaonyesha yule aliyemtaka kati ya Makardinali, P
Kukutana kwao Castel Gandolfo, unatajwa kuwa ni mwanzo wa majadiliano ya ana kwa ana kati ya Papa Francis na mstaafu Baba Mtakatifu Benedikto XV1, katika mwanga wa mwanga wa Roho wa Mtakatifu anawaongoza, katika utendaji wa matukio ya kipindi hiki.

Pia yanakumbukwa maneno ya Papa Francis kwa Makardinali juu ya mtagulizi wake Benedikto XVI, aliporudia kusema, "bado nina mawazo na upendo mkubwa uliojaa shukurani nyingi , na heshima zote kwa mtangulizi wangu Papa Benedict XVI, ambaye katika miaka ya utawala wake wa Kipapa, ameweza kulitajirisha Kanisa kwa mafundisho, wema, uongozi, imani, , unyenyekevu na upole. Hivi vinaabaki kuwa ni urithi wa kiroho kwa kila mtu"!
Papa Francesco, katika hotuba yake kwa aliendelea kusema, "katika mpanuko wa huduma ya utume wa Petro, tunapaswa kuishi kwa moyo wa majitoleo ya jumla, na Benedikto XV1, alilitafasiri hili , kwa busara na unyenyekevu, na kwa macho yaliyoitazama sana sura ya Kristu , Kristu Mfufuka na hai katika Ekaristi. Hivyo na atusindikiza daima kuptia sala zake, nasi tunamtolea shukurano zetu zisizo pimika, wala kuwa na ukoma katika hisia zetu.
Papa alieleza na kuendeela kuomba , ili kwamba, ukaribu wa Mstaafu Benedikti XVI, uliomo ndani ya mioyo yetu, uwe ni mwali wa moto unaoendelea kuwaka na kulishwa na sala zake, kwa ajili ya kusaidia Kanisa katika mambo ya kiroho na kazi za Kitume( Ni maneno ya Papa Francesco, kwa Makardinali wote, Machi 15, 2013).









All the contents on this site are copyrighted ©.