Ijumaa hii majira ya saa za asubuhi, katika chumba cha Mikutano,katika jengo la Kipapa
, Baba Mtakatifu Francis, alikutana na Mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali kwa
Jimbo Takatifu, ikiwa ni mara yake ya kwanza kukutana na mabalozi hao tangu azindue
utume wake katika kiti cha Petro, Jumanne ya wiki hii. Kwa niaba ya Mabalozi wote,
Salaam za Mabalozi kwa Papa, ziliwasilishwa na Balozi Mheshimiwa Jean-Claude Michel,
ambaye ni mwakilishi wa Ufalme wa Monaco, katika Jimbo Takatifu, ambaye kwa wakati
huu ni Mkuu wa zamu katika chombo kinacho waunganisha Mabalozi. Kwa wakati huu Jimbo
la Papa lina mahusiano ya Kidplomasia na mataifa 180. Papa aliianza hotuba yake
kwa Mabalozi , na salaam za shukurani za dhati kwa Waheshimiwa wote , Mabibi na Mabwana,akiutaja
wakati huo, kuwa ni nafasi au mwanya mzuri wa kubadilishana salaam za matashi mema
na mawazo katika namna ya kawaida, huku ndani mwake, akiwa bado na hisia hai za
wakati wa sherehe ya kuzindua kazi na utume wake wa Kipapa, ambamo kwa namna fulani,
iliyo toa picha kwamba, Utume wa Kipapa ni kwa ajili ya dunia nzima. Na sasa uwepo
wa Mabalozi hao, pia alijisikia kuwa karibu na watu wote wanao wawakilisha, katika
kushirikishana furaha na matatizo , matazamio na hamu zao. Na kwamba , uwepo
wa Idadi hii kubwa ya Mabalozi ni ishara kwamba, mahusiano kati ya nchi zao na Jimbo
la Takatifu, yana matunda mazuri na yenye faida kwa wanadamu. Alitaja kwa hakika
hilo ndilo lengo na tazamio kubwa kwa Jimbo Takatifu, uwepo wa mazuri kwa ajili
ya kila binadmau duniani. Na ni kwa uelewa huo, kwamba Askofu wa Roma , anaanza utume
wake, kwa kuweka matumaini yake katika uwepo wa urafiki na maelewano na nchi wanazo
wakilisha, na uhakika kwamba wanashirikishana katika lengo hili la kujenga urafiki.
Na wakati huohuo , pia ameonyesha kuwa na matumaini ya kupatikana nafasi, wakati huu
anapoianza safari hii ya utume wake , ya kwua na mawasiliano na mataifa machache
ambayo bado hayajaweka mkataba wa mahusiano ya Kidiplomasia na Jimbo Takatifu, ambayo
baadhi yake yalikuwepo wakati wa Ibada ya Misa kwa ajili ya kuzindua utume wake. Na
pia wale waliotuma ujumbe wao kama ishara ya ukaribu wao. Kwao wote amewashukuru
kwa dhati kwa hilo. . Na kwa mara ingine , Papa Francis alirudia, kuwaeleza
Mabalozi kwa nini amechagua jina la Francis, mtu maarufu nchini Italia na Ulaya ,
hata kwa watu wasiokuwa wafuasi wa Kanisa Katoliki , kwamba Francis aliyaacha maisha
ya kifahali na kuchagua maisha ya mtu maskini wa mitaani. Papa amehoji, ni
watu wangapi leo hii ambao bado wanaisha katika hali ya umaskini dunia! Na kwa jinsi
gani wanavumilia mateso haya makali. Alileleza hilo na kutaja mfano wa Francis wa
Assisi, akisema, Kanisa ssehemu mbalimbali za dunia, hujitahidi kuyafuta maisha
haya ya Francis kupitia utendajiw a vyombo vyake mbalimbali, vinavyo shughulika na
kujali hali za watu mbambali wanao kabiliwa na mateso haya, ambao ni wazi wako katika
nchi nyingi, kama wanavyoweza kushuhudia, matendo ya ukarimu unaofanywa na Wakristo,
wanao jitolea kusaidia wagonjwa, yatima, wasio na makazi na wanyonge waliosahaliwa
na kutengwa pembezoni , wakihangaika kuijenga jamii katika ubinadamu zaidi na haki
zaidi.
Pamoja na hilo Papa Francis ameasa kwamba, pia kuna aina nyingine
ya umaskini! Ni umaskini wa kiroho wa wakati wetu, ambayo unaathiri hasa nchi zinazoitwa
mataifa tajiri. Ni kile mtagulizi wake Mpendwa Benedict XVI, ilicho kiita "ukorofi
wa ukana Mungu , wenye kuona mambo yote ni ya mpito “, binadamu akijiamini kuwa
na uwezo kwa yote na hivyo kuhatarisha mshikamano wa watu. Na hiyo ni sababu ya pili
ya kuchagua jina la Francis. Francis wa Assisi, hata leo hii, anatuambia sisi kwamba
, lkazi ya kujenga amani ni ya lazima. Lakini, hakuna amani ya kweli bila ukweli!
Na haiwezekani kuwa na amani ya kweli, ikiwa kila mtu anajiona amejikamilisha mwenyewe,
na kupuuza utendaji wa mema kwa ajili ya wengine . Kila mtu anapaswa kukumbuka kwamba
ni asili msingi ya kila mtu, kuungana na kuwa na mshikamano na binadamu wengine.
Papa aliendelea kueleza , Moja ya cheo cha Askofu wa Roma, Baba Mtakatifu, Mjenzi
wa madaraja kati ya Mungu na watu. Na hivyo alionyesha matumaini yake kwamba, mazungumzo
kati yao, lazima yataweza kuwa msaada katika ujenzi wa madaraja ya kuunganisha watu
wote, kwa namna ambayo kila mtu anaweza kumwona mwingine si adui, au si mpinzani,
lakini ndugu, kaka au dada, anayepaswa kupokelewa na kukubatiwa. Kwa maana hiyo,
asili ya kazi yake inamsukuma kuwa mjenzi wa madaraja, kutoka pande zote za dunia,
ambazo kwa wakati huu, zimezidi kukaribiana na kutegemeana zaidi katika hitaji la
kukutana na kutengeneza nafazi za wazi zaidi kwa ajili ya mshikamano na udugu wa
kweli. Kwa ajili ya kazi hii, utendaji wa kidini, unakuwa msingi. Haiwezekani
kujenga madaraja kati ya watu na kumsahau Mungu. Na kinyume chake pia ni ukweli,
haiwezekani kuwa na mahusiano ya karibu na Mungu na kuwapuuza watu wengine. Kwa hiyo
ni muhimu kuimarisha mazungumzo kati ya dini mbalimbali, na Papa anafikiria hasa mazungumzo
na Uislamu. Papa ameendelea kueleza kwamba, alifurahia sana uwepo wa viongozi
wengi wa kiraia na kidini kutoka ulimwengu wa Kiislamu, wakati wa Ibada ya Misa ya
kuzindua Utume wake. Na pia ni muhimu kuimarisha haja ya kuwafikia wasio waumini,
hivyo kwamba tofauti zinazotenganisha na kuuumiza ubiadamu zisiendelee kuwepo. Badala
yake itawala hamu ya kujenga madaraja ya urafiki wa kweli kati ya watu wote licha
ya utafuti wao. Kupambana na umaskini, katika yote mawili kihali na kiroho ,
ujenzi wa amani na madaraja haya, kama ilivyokuwa, awali, vinakuwa ni vituo rejea,
katika safari yake ya Kitume aliyoianza, kwa kutoa wito na mwaliko kwa kila nchi
iliyo wakilishwa ,kujiunga. Na ameonyakwamba, safari hii, inaweza kuwa safari ngumu,
iwapo hawata jifunza kukua katika upendo kwa ajili ya dunia hii. Hili linasaidia
pia kufikiria jina la Francis, ambaye anatufundisha kuwa na heshima kubwa kwa uumbaji
mzima na katika kuwa walinzi wa mazingira yetu, ambayo mara nyingi, badala ya kutumika
kwa ajili ya mema ya wote, wachache wanakuwa tabia za uyonyaji na uchoyo binafsi,
usiojali madhara na hasara zinazo tokea kwa wengine.
Papa Francis , alimalizia
hotuba yake , kwa kuwashukuru Mabalozi wote wanaofanyakazi sambamba na Sekretariati
ya Nchi ya Vatican, kwa kazi ya kujenga amani na madaraja ya urafiki na udugu. Kupitia
kwao, alitoa tena shukurani zake za dhati kwa ushiriki wao katika maadhimisho ya juu
ya tukio la kuchaguliwa kwake, na alionyesha tena hamu yake ya dhati katika jitihada
za kazi kwa ajili ya kutoa matunda ya mema. Na mwisho aliwapa baraka zake za Kipapa
akiwaombea neema tele za Mungu ziwafikie wao na familia zao na watu wao wanao wawakilisha
Asante!