Wakristu Uarabuni , wafuahia kuundwa kwa Baraza la Kiekumene ...
Kuzaliwa kwa Baraza la Makanisa ya Kikristu nchini Misiri, inatajwa kuwa hatua muhimu
ya kiekumeni na msingi kwa Wakristu wa Misri. Baraza hili liliundwa mwishoni mwa
Wiki ya Sala ya Kuombea Umoja wa Wakristu wiki lililokamilika a tarehe 10 Februari,
kutokana na kuahirishwa katika tarehe zake , kwa sababu za machafuko ya kisiasa Misri.
Askofu Mouneer Hanna Anis, Askofu wa Dayosisi ya Kianglikana Misri, Afrika
Kaskazini na Pembe ya Afrika, ameeleza, kuundwa kwa Baraza la Makanisa la Kikristo
hivi karibuni ni tumaini kubwa katika uwepo wa umoja wa Wakristu katika nchi za kiarabu.
..Baraza hilo ni chombo cha ushauri, na kimefanikishwa kuanzishwa kwa juhudi za
Patriaki Tawadros II wa Kanisa la Kiotodosi.
Kulingana na Askofu Anis, pia
Mkuu wa Dayosisi ya Kianglikani ya Yerusalemu na Mashariki ya Kati, pia ametoa mchango
mkubwa na muhimu katika kufanikisha juhudi hizi za kuonyesha uwepo wa makanisa na
jumuiya za Kikristu katika mataifa haya ya kiarabu, na hivyo wanapaswa kuunganisha
nguvu kama jumuiya moja ya Kanisa, kukabiliana na changamoto nyingi zinazo wakabili
wakati huu wa hali ya sasa ya mivutano kuongezeka, baada ya utawala wa Husein Mubarak.
Mkutano wa kwanza wa Baraza ulifanyika mwezi uliopita na katika Kanisa Kuu
la Kanisa St Mark Coptic Orthodox, ambalo huchukuliwa kama Kanisa Mama katika Makanisa
ya Misri.. Katika mkutano huo, wawakilishi wa kutoka Makanisa matano na jumuiya
zote za Kanisa, zilihudhuria, waotodosi, Waanglikani, Wakoputiki, Wakatoliki, kutoka
makanisa ya kiinjili na makanisa ya Kigiriki pia.
Lengo lake la kwanza la
Mkutano kama alivyoeleza Askofu Katoliki la Kikoputiki , Assiut Kiryllos William,
ilikuwa ni kuimarisha uhusiano wa upendo na roho ya ushirikiano kati ya makanisa
wanachama. Ni kuwa na Mwili mpya wa Kanisa Uarabuni. Askofu wa Assiut Kiryllos William,
wakati akihojiwa na shirika la habari la Fides alieleza hayo na kuongeza kwamba chombo
hicho kitawasaidia kutembea pamoja katika njia ya uekumene na katika kuwa na msimamo
wa pamoja katika mazungumzo na mshikamano na jumuiya zingine zisizo za kikristo. Hii
ni fursa nyingine ya kukuza mipango ya pamoja hata kijamii na kitamaduni.
Hata
hivyo, aliongeza, lengo sio kutafuta mamlaka ya kisiasa, lakini ni mshikamano wa ndani
wa maisha ya makanisa na mtu binafsi.