Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza siku ya tarehe 20 Machi 2013 imeadhimisha Siku
ya Furaha Kimataifa, baada ya kupigiwa kura na hatimaye, kupitishwa na nchi wanachama
193 wa Umoja wa Mataifa. Licha ya taabu, mahangaiko na hali ya kukata tamaa inayowakabili
watu kutoka sehemu mbali mbali za dunia, lakini pia Jumuiya ya Kimataifa walau inaweza
kuonesha furaha hata kwa dakika chache.
Hii inaweza kuwa ni furaha inayofumbatwa
kitaifa, katika Jamii, mahali pa kazi, lakini zaidi katika Familia, ambayo kweli inapaswa
kuwa ni chimbuko na chemchemi ya furaha; lakini wakati mwingine mambo yanakwenda
kinyume na matarajio ya wengi.
Kila mtu anachangamotishwa kuwa ni sababu ya
furaha na faraja kwa jirani yake, kama alivyosema Baba Mtakatifu Francisko kwa waamini
na watu wote wenye mapenzi mema.