Upembuzi yakinifu kuhusu matumizi ya wanajeshi wa kukodiwa na makampuni binafsi ya
ulinzi katika migogoro ya kivita!
Umoja wa Mataifa unafanya upembuzi yakinifu kuhusu matumizi ya wanajeshi wa kukodiwa
na makapuni binafsi ya ulinzi na matokeo ya utafiti huu yanatarajiwa kuwasilishwa
kwenye Mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika mwaka 2014.
Haya yamesemwa
na Bwana Anton Katz, mtaalam wa masuala ya haki msingi za binadamu anayefanya kazi
kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa, baada ya mkutano wao uliofanyika hivi karibuni
mjini Geneva.
Kumekuwepo na ongezeko kubwa la wanajeshi wa kukodiwa na makampuni
binafsi ya ulinzi ambayo kwa sasa yanafanya kazi katika soko la kimataifa, hali ambayo
imechangia kwa kiasi kikubwa kinzani na migogoro ya kivita inayoendelea katika nchi
kama vile Syria. Nchi kama Ghana, Mauritius na Togo kutoka Afrika zinataka kufahamu
watu wanaojihusisha na biashara hii, ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.