2013-03-20 15:12:31

Tuko bega wa bega na Papa Francis- WUCWO


Wanachama wa Muungano wa Dunia wa Mashirika ya Katoliki ya Wanawake (WUCWO), wametuma ujumbe wao, kufuatia homilia ya Papa aliyoitoa wakati wa Ibada ya Misa ya kuzindua utume wake siklu ya Jumanne, 19 March 2013.
WUCWO, wanasema, “Tumeshuhudia tukio la kihistoria na kuuishi uzoefu wa ajabu, ambao daima utabaki katika mioyo yetu na katika kumbukumbu zetu. Mungu ametubariki sote kwa kuwa na mchungaji mpya, Papa Francis! Hata jina lake linatuongezea sisi amani na haja ya kujali viumbe wote wa Mungu. Kweli huu ni wakati wa furaha, furaha kamili katika tumaini na ahadi".
Ujumbe unaendelea kusema, Wanachama wa WUCWO, wameichambua kwa makini na homilia ya Papa, na kuiona, kwa kanisa ina mambo muhimu matatu ya kufanyia kazi, nayo ni kanis akama mhujaji, Kanisa mjenzi wa jamii bora na kanisa mwenezaji wa Injili ya Upendo kuokoa wa Kristu.
WUCWO , lilianzishwa mwaka 1910, na imekuwa katika hija kwa zaidi ya miaka 100, kwa lengo la kukuza uwepo, ushiriki na uwajibikaji wa wanawake Katoliki katika jamii na kanisa, ili kuwawezesha kutimiza kazi yao ya uinjilishaji na kufanikisha maendeleo ya binadamu. Na ina nia za kuendelea kufanya kazi bila kuchoka katika ushirika na Baba Mtakatifu Francis, na wanawake wote na watu wa mapenzi mema ili kujenga jumuiya bora ya kanisa, iliyo imarika katika kumkiri Kristu kupitia utendaji na huduma za kawaida kwa ajili Uinjilishaji Mpya.

Muungano huu huwashirikisha wanawake zaidi ya milioni 5 kutoka nchi 66, na hujali na liko tayari msaada unaohitajika kwa Papa Francis , kama kupunguza umaskini, kufanikisha maendeleo ya haki za binadamu kwa kuanza na haki ya msingi ya maisha, na kwa wote waathirika wa unyanyasaji, hasa waathirika wa biashara ya binadamu ambayo, Kardinali Bergoglio, Papa Mpya, alikwisha litamka hilo kwamba, ni dharirisho kwa hadhi ya wanawake".

Muungano wa Dunia wa Mashirika ya Katoliki ya Wanawake (WUCWO) pia unatoa majibu kwa maombi mazuri la Papa Francis, kwa kumhakikishia wingi wa sala zisizo na kipimo na msaada wote kwa ajili yake Utume wake wa kipapa.
Ujumbe huo umemalizia kwa kmwomba Mama Yetu Malikia wa Amani na Msimamizi wa WUCWO,Mama Bikira Maria, afikishe maombi yao kwa Mwana wa Mungu Yesu Kristu, ili daima awe karibu na Papa Francis, akimwongoza kwa upole na ukamilifu wote katika siku zake zote.








All the contents on this site are copyrighted ©.