2013-03-20 15:13:46

FAO, yaonesha tumaini kwa Papa Francis katika kupambana na njaa duniani


Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa, (FAO), limeonesha matumaini kwa Papa Francis kwamba, atakuwa msaada katika kupambana na njaa na ufukara wa kukithiri duniani . Tumaini hilo kumetajwa na Mkurugenzi Mkuu wa FAO, Bwana Jose Graziano da' Silva, wakati akihudhuria Ibada ya Uzinduzi wa Kazi za Kitume za Papa Francis, siku ya Jumanne.
Mkurugenzi Mkuu wa FAO Jose Graziano anamwona Papa Francis kama "rafiki wa maskini, na hivyo bila shaka atajiunga katika barabara ya kupambana dhidi ya njaa, utapiamlo na umaskini uliokithiri.

Graziano da Silva alihudhuria sherehe kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, na alijiunga na waheshimiwa wengine na makundi ya wajwakilishi wa mashirika na jumuiya, waliokusanyika katika uwanja wa Kanisa Kuu la Mtaktifu Petro, mjini Vatican.

Graziono ameendelea kumtaja Papa Francis, kuwa bingwa katika utetezi wa haki na mahitaji ya walio katika mazingira magumu zaidi hasa watoto, wanawake na wanaume pia. Na pia alionyesha kufurahia kwamba, Papa Francis alichagua jina la Mtakatifu Francis wa Assisi, mwenye kujulikana kama rafiki wa maskini.

Pia alitaja , msaada wa Vatican na dini nyingine ni muhimu katika jitihada za kutokomeza njaa na ujenzi wa mustakabali endelevu, na uboreshaji wa maisha ya mazingira magumu zaidi kati yetu. Juhudi hizi si tu kufanyika katika hisia za kisiasa na kiuchumi, lakini pia ni muhimu kimaadili na ni haki , alieleza Graziano da Silva.

Katika maelezo haya, aliendelea kutoa pongezi kwa Papa Francis na pia mtangulizi wake, Mstaafu Papa Benedict XVI, kwa msaada wao katika mapambano dhidi ya njaa na, hasa, jitihada za kutetea hatua zinazolenga kupunguza makali ya jaa na kmfumko wa bei za bidhaa katika soko la dunia.









All the contents on this site are copyrighted ©.