2013-03-20 15:37:55

Familia -shule ya upendo na fadhila- Askofu Mkuu Paglia


Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Familia, Msgr. Vincenzo Paglia, Jumatatu alishiriki katika Mkutano uliaondaliwa na Tume ya Utazamaji wa kudumu katika Umoja wa Mataifa , pamoja na mashirika mengine ya kimataifa yenye makao yake Geneva, juu ya mada: "Kukuza haki za binadamu na uhuru kisheria na kijamii , ulinzi wa familia .

Kazi za Mkutano huo ziliwasilishwa na Askofu Mkuu Silvano M. Tomasi, Mjumbe Mtazamaji wa Kudumu wa Jimbo Takatifu, katika ofisi za Umoja wa Mataifa za Geneva. Mratibu wa Mkutano huo akiwa Mjumbe Mwakilishi wa Kudumu wa Ufalme wa Swaziland (Kusini mwa Afrika), Thembayena Annastasia Dlamini.


Wazungumzaji wakiwa Msgr. Nyasi: Prof Xavier Lacroix, profesa katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki Lyon na mjumbe wa Kamati ya Taifa ya Ushauri juu ya Maadili katika Ufaransa, na Michael Schumacher, mtafiti katika Chuo Kikuu cha Fribourg, Switzerland.


Askofu Vincenzo Paglia aliwasilisha mandhari: "rasilimali ya familia kwa Jamii, katika mtazamo wa Mwaka 20 wa Familia Kimataifa" na Maadhimisho ya thelathini ya Mkataba wa Haki za Uzazi wa Jimbo Takatifu.


Rais wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Familia, akitoa utangulizi katika mkutano huo aliwaambia , tukio hili la kuadhimisha miaka 20 ya Familia Kimataifa, na Idara ya Uchumi na Jamii ya Baraza la Uchumi na Jamii la Umoja wa Mataifa kwa mwaka huu, ni fursa nyingine , katika kutazama uzito wa jukumu la familia katika maendeleo, ikiwa ni pamoja na kushirikishana uzoefu na utendaji wa sera nzuri kwa ajili ya familia, kwa kuzingatia mabadiliko katika dhana ya familia na kupendekeza ufumbuzi.

Askofu Mkuu Vincenzo amesisitiza , familia ni msingi wa haki za binaadamu. Familia ni kitengo msingi cha ubinadamu katika wa jamii. Katika familia, vizazi hukutana, kupendana, kuelimisha, kusaidiana na kuishi pamoja katika hali za mpito kutoka umri mmoja hadi mwingine. Na dhana hii ya familia ni utendaji asilia wa tamaduni zote katika historia, kama inavyotambuliwa katika Azimio la Haki za Binadamu: "Wanaume na wanawake wa umri wote, bila mipaka ya utaifa au dini au rangi , wote wana haki ya kuoana na kuuunda familia ya mke na mme '.

Hivyo, "familia ni rasilimali ya msingi ya jamii na msingi wa ukuu wa utu na ubinadamu, wenye kujenga utulivu mkono kwa mkono, na hivyo uwepo wa jamii tulivu katika mtiririko wake. Ndoa ya mke na mme ambayo ndiyo mwanzo wa familia inakuwa ni kitendo cha thamani sana katika jamii, ambacho daima huongeza ubora wa uhusiano kati ya wanandoa.
Ndoa, kama haikusimikwa vyema, huweza kuwa na athari nyingi kwa mtu , kibaiolojia, kisaikolojia, kiuchumi na kijamii pia , si kwa watoto tu lakini hata watu wazima wenyewe Kwa mtazamo huo, utulivu wa mahusiano ya familia , utulivu wa ndoa ni muhimu sana katiak mafanikio ya mtu binafsi na masuala chanya ya kijamii.








All the contents on this site are copyrighted ©.