2013-03-19 14:31:40

Baba Mtakatifu Francis azindua utume wake kwa Ibada ya Misa


Jumanne hii majira ya asubuhi, Baba Mtakatifu Francis, amezindua rasmi utume na uongozi wake kwa Ibada ya Misa Takatifu kwenye Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro , hapa Vatican. Papa ameongoza Ibada hii akisaidiana na Makardinali na Maaskofu wapatao 180 na kuhudhuriwa na Wakuu wa nchi 31 , Viongozi wa Kifalme 6 , Wana Wafalme 3 , Mawaziri Wakuu 11. Na kumekuwa na umati wa watu wasiopungua 200, 000, watu wa dini na tamaduni zote. .

Kabla ya Ibada, Papa akiwa ndani ya gari la Kipapa jeupe la wazi, aliwasiri katika uwanja huu, ambako alipita katika vijia vilivyoandaliwa kuzungukia kwa ajili ya kusalimia watu wa kariba na dini zote, waliokuwa wakimsubiri kwa hamu, kabla ya kuanza Ibada. Mara baada ya zoezi hilo, aliingia ndani ya Sakrastia kwa ajili ya maandalizi ya kuanza Ibada, ya Maadhimisho ya Siku Kuu ya Yosefu Mchumba wa Maria na mlinzi wa Kanisa la Ulimwengu, na pia kwa nia ya kuzindua utume wa kazi zake kama khalifa wa mtume Petro.

Papa Francis, akiwa mrithi wa Mtakatifu Petro wa 265, aliiianza Ibada hii kwa kuteremka chini katika Kaburi la Mtakatifu Petro , kama yalivyo mapokeo ya tangu kale, akiwa ameandamana na Mapatriaki wa Makanisa ya Mashariki ambako kwa muda walitolea sala na kufukiza ubani wa kitume.

Baada ya ya hapo , Papa alijiunga katika maandamano ya kuanza Ibada katika uwanjani wa kanisa Kuu. , huku sala na maombi mbalimbali yakitolewa......."kwa Papa Francis Kuhani Mkuu na Askofu wa Roma, ambaye leo hii anauanza utume wake, mjalie nguvu na uelewa wa Roho Mtakatifu kwa ajili ya umoja wa Kanisa la Ulimwengu"......

Katika Ibada hii ya kipekee, Papa Francis, kama Mkuu wa Kanisa la Kristu, khalifa wa mtume Petro na Askofu wa Roma, alivalishwa Paullium na Pete ya Petro, ishara ya kuuanza Utume wake..."Wewe ni Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga Kanisa langu na milango ya kuzimu kamwe haitakuzuia . Nitakupa Ufunguo za Ufalme wa Mbingu"........

Palium aliyovaaa Papa , imetengenezwa kwa mayoya ya kondoo , kama ishara ya Askofu na Mchungaji mwema wa kondoo. Pallium hiyo, juu yake kuna misalaba sita midogo mwekundu, ikiashiria alama ya mwana kondoo aliyesulubiwa kwa ajili ya wokovu wa binadamu. Na hivyo inakuwa tofauti kidogo na Pallium wanayovalishwa Maaskofu Wakuu ambayo huvaa pallium yenye misalaba midogo sita mweusi inayoashiria mwana kondoo mpotevu na dhaifu anayebebwa mabegani na kupelekwa katika maji ya uzima .

Wakati Papa akiwavlishwa Pallium manaeno haya yalisema, Mungu wa amani , aliyemfufua kutoka katika wafu Bwana wetu Yesu Kristu, Mchungaji Mkuu wa wanakondoo na akuvalishe Pallium hii iliyo inayotoka katika Kaburi la Mtakatifu Petro.



Mchungaji mwema aliyempa Petro mamlaka ya kulisha wana kondoo wake. Leo hii wewe unakuwa mrithi wa Petro, kama Askofu wa Kanisa hili ambamo Mtume Petro na Paulo walikuwa ni Mababa wa Imani.

Roho wa Ukweli , anayetoka kwa Baba na akijualie wingi wa zawadi ya hekima na maarifa katika kuzitenda kazi zake za kitume na hasa katika kuwaimarisha waamini kiroho na katika umoja wa Kanisa. .......

Baada ya kuvalishwa Pallium, Papa alivalishwa Pete ya Petro. Pete inayoitwa Pete ya mvuvi , kwa sababu Petro Mtume alikuwa ni Mvuvi. Petro baada ya kumwamini Kristu, alifanywa kuwa mvuvi wa watu na Kristu mwenyewe. Na hivyo unakuwa ni wito kwa Mkhalifa wote wa Mtume Petro, kuwa mstari wa mbele kuteka nyavu za Injili ya wokovu kilindini, kuvua wake kwa waume kwa Injili ya Kristu.

Papa alivalishwa Pete ya Petro na Kardinali Angelo Sodano , ikifuatiwa na sala " , Kristu Mwana wa Mungu aliyehai , Mchungaji na Mlinzi wa roho zetu, aliyelijenga kanisa lake juu ya mwamba huu, anakupatia pete ya Petro iliyotiwa muhuri wa Peter Mvuvi wa Galilea, ambaye Bwana alimpa dhamana ya kutunza funguo za Ufalme wa Mbinguni.

Leo hii, unakuwa Khalifa wa Mtume Petro , Askofu wa kwanza wa Kanisa lilojengwa katika umoja wa Upendo , kama Mtume Paulo pia alivyofundisha. Roho wa Upendo na amiminwe ndani ya mioyo yetu , na akujalie upole na uimara wa kudumisha kupitia utume wako, wale wote wanaosadiki katika ushariki wa Kristu". ......

Pia Makardinali wawili kwa niaba ya dekania ya Makardinali wote walionyesha heshima na utii wao kwa Papa mpya Francis kwa maneno , , Wewe ni Petro na juu ya mwamba huu, nitalijenga Kanisa langu , na milango ua kuzimu haitakuzia. Nitakupa funguo za Ufalme wa Mbingu . Kila utakalo liruhusu duniani na mbinguni litabarikiwa na kila utakalo lifunga duniani na mbinuni litafungwa .

Kilichofuatia ni Liturujia ya Neno, masomo yaliyoandaliwa kwa ajili ya Siku Kuu Mtakatifu Yosef, Mchumba wa Bikira Maria. Somo la kwanza kutoka Kitabu cha Samweli 7, 4-5, 12-14. 16 , Somo la pili kutoka Barua ya Mtume Paulo kwa Warumi 4: 13,16-18.22 na Somo la Injili ya Marko 1:16, 18-21, 24 a.








All the contents on this site are copyrighted ©.