Wananchi wa Zimbabwe wapiga kura ya maoni kwa amani na utulivu
Wananchi wa Zimbabwe, wapatao millioni mbili, Jumamosi tarehe 16 Machi 2013 walipiga
kura ya maoni kuhusu Katiba Mpya ya Zimbabwe inayopania kupunguza madaraka ya Rais
na kuimarisha utawala wa sheria na haki msingi za binadamu.
Akizungumzia kuhusu
mwitiko wa wananchi katika mchakato wa kupiga kura ya maoni, Jaji Rita Makarau kutoka
Tume ya Uchaguzi alisema kwamba, wananchi wachache wamejitokeza kupiga kura katika
vituo 9,400 vilivyokuwa vimepangwa. Zimbabawe ina wananchi millioni 6.6 waliokuwa
wamejiandikisha kupiga kura ya maoni, ingawa vyama vikuu vya kisiasa vilikuwa vimekubali
kushiriki katika mchakato wa kupiga kura.
Zoezi la kuhesabu kura za maoni
limeanza na linatarajiwa kukamilika walau baada ya siku tano. Wananchi wengi wameshiriki
kwa amani na utulivu.