Unyanyasaji wa kijinsia ni kosa la jinai linalopaswa kushughulikiwa kisheria
Kardinali Wilfrid Fox Napier wa Jimbo kuu la Durban, Afrika ya Kusini, ameomba msamaha
kwa wote walioguswa na kutendewa na kauli yake kwamba, watu wanaofanya vitendo vya
unyanyasaji wa kijinsia na ni wagonjwa na wanahitaji kupewa tiba, bila ya kukazia
kwamba, ni vitendo vya jinai ambavyo vinapaswa kushughulikiwa kisheria.
Kardinali
Napier anasema, pengine Kanisa Katoliki halikutoa uzito mkubwa kwa vitendo vya unyanyasaji
wa kijinsia pamoja na kuchukua hatua za kuvikomesha, kwani madhara yake yamekuwa ni
makubwa mno katika maisha na utume wa Kanisa, sehemu mbali mbali za dunia. Watu walionyanyaswa
kijinsia wanahaki ya kupata msaada wa hali na mali kutoka kwa Kanisa, wanapojitahidi
kuponya madonda na maumivu yao ya ndani.