2013-03-18 07:37:59

Uganda yampongeza Papa Francis


Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameungana na wakuu mbali mbali wa nchi na Jumuiya ya Kimataifa wanaoendelea kutuma salam za matashi mema kwa Baba Mtakatifu Francis kwa kuchaguliwa kwake kuliongoza Kanisa Katoliki lenye waamini zaidi ya Billioni 1.2, walioenea sehemu mbali mbali za dunia.

Rais Museven anatambua na kuthamini mchango uliotolewa na Baba Mtakatifu Francis ambaye kwa sasa wengi wanamwita Baba Mtakatifu wa Maskini, katika maisha yake. Anamwomba, atumie uzoefu na mang’amuzi yake kutoka katika nchi za kimissionari ili kuleta mabadiliko ndani ya Kanisa.

Lakini, hata hivyo Rais Museveni habainisha wazi wazi mabadiliko ambayo angependa Baba Mtakatifu Francis ayafanye kwa ajili ya ustawi, mafao na maendeleo ya Kanisa na Jamii kwa ujumla.








All the contents on this site are copyrighted ©.