2013-03-18 16:26:00

Mamia ya maelfu watarajiwa kuhudhuria Ibada ya Papa Francis kuzindua utawala wake wa kitume, Jumanne: Hakuna kiingilio wala tiketi.


Siku ya Jumanne Machi 19, 2013, ambamo Mama Kanisa ana adhimisha Siku Kuu ya Mtakatifu Yosefu Mchumba wa Bikira Maria, na Msimamizi wa Kanisa la Ulimwengu, majira ya asubuhi ya saa tatu na nusu za asubuhi, (saa za Roma), Papa Francis, ataongoza Ibada ya Misa Takatifu , kama alama rasmi ya kuzindua utume na utawale wake wa Kipapa katika kiti cha Mtume Petro.

Mamia ya maelfu ya mahujaji na wageni wanatarajiwa kuujaza uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, kwa ajili hiyo. waamini wote mnatagaziwa kwamba Ibada hii ni wazi kwa wote na hakuna haja ya kuwa na tiketi kama kiingilio.

Ibada hii, itatangazwa moja kwa moja na vituo vingi vya redio, televisheni na njia nyingine za mpya za mawasiliano, kama itakavyo sikika moja kwa moja pia katika tovuti za Radio Vatican.
Katika Ibada hii, viongozi na Wajumbe rasmi wa viongozi wa kidini na kisiasa watakuwepo.Vivyo hivyo Makardinali wote, Maaskofu Wakuu na Maaskofu kadhaa kutoka pande mbalimbali za dunia, wameteuliwa kuja kuwakilisha makanisa mahalia na kuionyesdha sura ya kanisa la Kanisa la Ulimwengu.
Na kwamba Patriaki wa Kiekuemeni wa Constantinople, Bartholomayo I, ambaye ni huchukuliwa katika nafasi sawa na Papa katika Usharika wa Kanisa la Kiotodosi la Mashariki,pia anatarajia kuandika historia ya mpya ya kushiriki ibada hii kwa mara ya kwanza. Na Jumuiya ya Kianglikani duniani , inawakilishwa na Askofu Mkuu wa York Uingereza , Dr. John Sentamu, anayemwakilishi kiongozi mkuu wa Jumuiya hiyo, Askofu Mkuu wa Canterbury, kama itakavyo kuwa pia uwepo wawakilishi wa imani na tamaduni zingine kubwa duniani.
Kwa dunia ya Kisiasa , kati ya wanaotarajiwa kuwepo ni pamoja na Rais wa Argentina Cristina Kirchner, pia Rais Dilma Rousseff Rais wa Brazil, na Rais Enrique Peña Nieto, Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, na Mwana Mfalme wa Uingereza anayemwakilisha Malkia Elizabeth 11 . Rais Obama wa Marekani anawakilishwa na Makamu wake Joe Biden, na Gavana Mkuu wa Canada, Daudi Johnston.
Wengine watakao kuwepo katika uzinduzi huu, ni pamoja na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean-Marc Ayrault na Waziri Mkuu-Waziri Mariano Rajoy wa Hispania. Na Rais wa Baraza la Ulaya, Herman Van Rompuy, na Rais wa Tume ya Ulaya, José Manuel Barroso, wote wameonyesha nia za kuhudhuria, kwa kutaja wachache.
Papa Francis , anazindua kazi zake kama Askofu wa Roma na Mkuu wa Kanisa Katoliki la ulimwengu baada ya kuchaguliwa na Makardinali siku ya Jumatano illiyopita katika kura ya siri iliyopigwa kikao cha Conlave, nyakati za jioni. Na Ibada hii ya Jumanne , ni alama ya mwanzo kabisa ya utawala wake kama khalifa wa Mtume Petro.








All the contents on this site are copyrighted ©.