2013-03-16 16:54:16

Wakuu wa Mabaraza ya Kipapa kuendelea na nyadhifa zao kwa sasa!


Baba Mtakatifu Francis ameamua kwamba, Marais na Wenyeviti pamoja na wajumbe wa Mabaraza ya Kipapa mjini Vatican wataendelea na shughuli zao, hadi hapo uamuzi mwingine utakapotolewa na Yeye mwenyewe. Taarifa hii pia inawahusu Makatibu wakuu wa Mabaraza haya.

Baba Mtakatifu Francis anasema, angependa kuchukua fursa hii kwanza kabisa kufanya tafakari ya kina, kusali na kujadiliana na wahusika wakuu kabla ya kusitisha au kuendeleza uteuzi uliokuwa umekwishafanyika. Kwa taarifa tu ni kwamba, Khalifa wa Mtakatifu anapotoka madarakani kwa kifo au kwa kung'atuka kama alivyofanya Baba Mtakatifu Benedikto wa kumi na sita, viongozi wote waliokuwa wanafanya utume wao kwenye Mabaraza ya Kipapa, nyadhifa zao zinakoma hadi uchaguzi wa Papa Mpya.







All the contents on this site are copyrighted ©.