2013-03-14 11:36:16

Salam za pongezi na Matashi mema kutoka katika Umoja wa Mataifa


Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Ban Ki-Moon amemtumia salam za matashi mema Baba Mtakatifu Francis kwa kuchaguliwa kwake kuliongoza Kanisa Katoliki. Ni matumaini yake kwamba, Umoja wa Mataifa utaendelea kushirikiana na Papa Francis, katika utekelezaji wa mchakato wa kutafuta na kudumisha misingi ya amani, haki jamii pamoja na haki msingi za binadamu, kama nguzo msingi za maendeleo endelevu.

Umoja wa Mataifa una amini kwamba, changamoto mbali mbali zinazojionesha duniani zinaweza kukabiliwa kwa njia ya majadiliano. Ni matumaini ya Bwana Ban Ki-Moon kwamba Baba Mtakatifu Francis ataendeleza urithi na utajiri mkubwa ulioachwa na Papa mstaafu Benedikto wa kumi na sita katika mchakato wa kuendeleza utamaduni wa mshikamano.







All the contents on this site are copyrighted ©.