Salam na matashi mema kwa Baba Mtakatifu Francis wa kwanza kutoka Argentina!
Dr. Cristina Fernandes de Kirchner, Rais wa Argentina, kwa niaba yake mwenyewe na
kwa niaba ya Serikali ya Argentina, amemtumia salam za matashi mema na pongezi Baba
Mtakatifu Francis kwa kuteuliwa kwake kuliongoza Kanisa Katoliki.
Ni matumaini
ya wananchi wa Argentina kwamba, Baba Mtakatifu ataweza kutekeleza wajibu na dhamana
yake kama Kiongozi wa Kanisa, utume ambao utamwezesha kuzaa matunda katika mchakato
wa kutafuta haki, amani, usawa na udugu kwa ajili ya binadamu wote.