2013-03-14 10:53:07

Matarajio ya Kiekumene baada ya uchaguzi wa Papa Francis


Patriaki Bartolomeo wa kwanza wa Kanisa la Kiorthodox la Costantinopoli amemtumia salam na matashi mema Baba Mtakatifu Francis, kwa kusema kwamba, huduma yake ya kitume kama Khalifa wa Mtakatifu Petro, itasaidia kudumisha mchakato wa kutafuta amani duniani pamoja na kuendeleza mapambano dhidi ya umaskini, magonjwa na ujinga.

Ni matumaini yake kwamba, Baba Mtakatifu Francis ataendeleza mchakato wa majadiliano ya kiekumene miongoni mwa Makanisa haya mawili.







All the contents on this site are copyrighted ©.