2013-03-14 11:56:32

Marekani itaendelea kushirikiana na Kanisa Katoliki kwa ajili ya mafao ya wengi!


Rais Barack Obama wa Marekani amemtumia, sala, salam na matashi mema Baba Mtakatifu Francis kwa kuchaguliwa kwake kuwa Khalifa wa Mtakatifu Petro. Rais Obama anamkumbuka sana Papa Francis kwa mshikamano na maskini pamoja na wote wanaosukumizwa pembezoni mwa Jamii.

Jina la Francis linaonesha na kugusa ule upendo na faraja ya Mungu kwa watu wake. Ni matumaini ya Serikali ya Marekani kwamba, itashirikiana kwa karibu na Baba Mtakatifu Francis kwa ajili ya kudumisha misingi ya haki, amani, usalama na utu wa kila mtu!

Makamu wa Rais Joe Biden anatarajiwa kuongoza ujumbe wa Serikali ya Marekani katika sherehe za kuanza kwa utume wa Papa Francis hapo tarehe 19 Machi 2013. Itakuwa ni fursa maalum kwa Bwana Joe Bin Laden kutoa salam na matashi mema kutoka kwa wananchi wa Marekani moja kwa moja kwa Baba Mtakatifu Francis.

Anasema, Kanisa Katoliki limekuwa na mchango mkubwa katika maisha yake na katika maisha ya mamillioni ya wananchi wa Marekani si tu katika masuala ya imani, haki, utu na heshima ya kila mwanadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu.







All the contents on this site are copyrighted ©.